Uncategorized

SIMBA QUEENS YAIPIGA MKONO YANGA PRINCESS

admin July 10, 2020 3:47 pm


TIMU ya Simba Queens leo imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wapinzani wake Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo wa leo, Julai 10, ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambapo Simba ilipata mabao hayo kupitia kwa Mwanahamisi Omary dakika ya 32 na 75 na
Oppah Clement dakika ya 65 na 82 ambao walifunga mabao mawilimawili huku bao jingine lilifungwa na Joelle Bukuru dakika ya 69.

Joel Nasri dakika ya 35 alipachika bao pekee la Yanga Princess ambayo imepanda ligi msimu uliopita ikiwa  haijabahatika kupata ushindi mbele ya Simba.

Zikiwa zimecheza mechi nne, Simba Queens imefunga jumla ya mabao 20 huku Yanga Princess ikifunga jumla ya mabao matatu.

BAADA YA KUANZA KWA KUCHECHEMEA, COASTAL UNION YAZINDUKA MUUAJI WA SIMBA APEWA JUKUMU LINGINE LA KUIMALIZA KWA MARA NYINGINE TENA TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply