Uncategorized

SIMBA QUEENS YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA PRINCESS LEO

admin July 10, 2020 8:47 am


MUSSA Mgosi, Kocha Mkuu wa timu ya Simba Queens amesema kuwa leo wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake utakaowakutanisha dhidi ya Yanga Princess.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo majira ya saa 10:00 jioni, Uwanja wa Simba Mo Arena.

Leo inakuwa ni mara ya nne kwa Simba Queens kumenyana na Yanga Princess kwenye mechi za ligi huku mechi zote tatu zilizopita Yanga ikikubali kufungwa jumla ya mabao 15 na huku wao wakifunga mabao mawili.

Mchezo wa kwanza, Yanga Princess ilifungwa mabao 7-0 na mzunguko wa pili ikafungwa mabao 5-1 kisha msimu huu mchezo wa kwanza Yanga Princess ikifungwa mabao 3-1.

Mgosi amesema:”Hakuna tunachohitaji zaidi ya pointi tatu uwanjani, tunatambua kwamba watakuja kuhitaji kushinda mbele yetu tutapambana.”

YANGA KUTUA DAR LEO KUENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA NYOTA MWINGINE, MTAMBO WA MABAO NDANI YA YANGA HATIHATI KUIKOSA SIMBA JULAI 12

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply