Uncategorized

KLOPP:TUTAFANYA KILA NJIA KUMPA HESHIMA HENDERSON

admin July 12, 2020 6:47 pm


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa nahodha wake Jordan Henderson licha ya kuwa ni majeruhi atapewa heshima kwa kuiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi Kuu ya England.

Liverpool, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England wanatarajiwa kukabidhiwa kombe hilo Julai 22 watakapokuwa wakimenyana na Chelsea Uwanja wa Anfield.

Liverpool imefanikiwa kutwaa taji hilo baada ya miaka 30 kumeguka bila kutwaa taji hilo na unakuwa ni ubingwa wao wa 19 hivyo wanaweka historia mpya.

Henderson yupo nje baada ya kupata majeraha ya goti kwenye mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Brighton.

“Tutafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba tunakuwa na mchezaji Henderson, tutahakisha anakuwa na nafasi ya kupata heshima yake kwa kubeba kombe hilo,” amesema.

SIMBA YAIPIGA YANGA 4G, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO MORRISON AZUA TAHARUKI TAIFA, AGOMEA KUKAA BENCHI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply