Uncategorized

NAMUNGO FC YAIPIGIA HESABU SIMBA, WALIWASOMA WAKATI WANAPAMBANA NA YANGA

admin July 13, 2020 9:47 pm

UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa una kazi kubwa ya kupambana na Simba kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela. 

Namungo FC ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars uliochezwa Julai 11, Uwanja wa Mkwakwani.

Itamenyana na Simba anbao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Bara waliopenya hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga.

Kocha Mkuu wa Namungo FC,  Hitimana Thiery amesema kuwa anatambua kuwa kuna kazi kubwa kupambana na mabingwa kwenye mchezo wao wa fainali. 

“Sio kazi nyepesi kushinda mbele ya mabingwa ambao wapo vizuri na tunawaheshimu kwa kuwa tunawatambua vizuri wapinzani wetu na wanajua kile wanachokifanya. 

” Nilikuwepo uwanjani kuona namna ambavyo walikuwa wakipambana ndani ya uwanja, ila hilo halinipi presha nitakiandaa kikosi kipate ushindi, ” amesema.

BAADA YA KUICHAPA YANGA JANA..BOCCO NA KAGERE WABEBA TUZO SOLSKJAER: SARE NI KIPIMO CHA UWEZO WA WACHEZAJI WANGU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply