INAELEZWA kuwa wachezaji na benchi la ufundi la Simba leo wamepewa mkwanja wao wa milioni 380 ambao waliahidiwa kupewa kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Yanga.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga mchezo uliochezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa, Dar.
Kabla ya mchezo awali ilielezwa kuwa kungekuwa na mgawanyiko kwa upande wa mkwanja huo kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na wale ambao wangekaa benchi pamoja na wengine ambao hawakucheza kabisa.
Jambo hilo lilipokelewa tofauti na wachezaji waliocheza mchezo huo na kuomba uongozi uwape wote fedha zinazolingana kwa kuwa ni timu moja.
Hivyo leo wachezaji wote wamevuta mkwanja wa milioni 10 kila mmoja ikiwa ni bonasi ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.
Simba itakutana na Namungo FC Kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela.
Katibu Mkuu wa Simba, Dr. Arnold Kashembe amesema kuwa suala la zawadi kwa wachezaji lipo ila litawekwa wazi wakati ukifika.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.