Uncategorized

OWEN CHAIMA AMUWAZIA MAKUBWA NCHIMBI WA YANGA

admin July 18, 2020 6:47 am


OWEN Chaima kipa namba moja ndani ya Klabu ya Singida United amesema kuwa anamuombea dua nyota wa Yanga, Ditram Nchimbi afike mbali Kwenye maisha yake ya soka.

Chaima amesema kuwa anaamini uwezo wa Nchimbi ni mkubwa hivyo akipambana zaidi anaweza kufikia malengo yake aliyojiwekea.

Walipokutana Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilikubali kichapo cha mabao 3-1.

“Ninamuombea kheri Nchimbi ni mchezaji mzuri nina amini atafika mbali akiongeza juhudi,” amesema.

Singida United tayari imeshashuka daraja baada ya kujikusanyia pointi 15 kibindoni leo ina kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI BAADA YA KUIBUKA TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED, YIKPE AFICHUA KILICHO NYUMA YA PAZIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply