Uncategorized

BERNARD MORRISON AIBUA MAPYA TENA YANGA

admin July 20, 2020 1:47 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison, ameibuka na jipya akisema kwamba, sababu kubwa ya yeye kutoenda mazoezini ni kuhofia kupigwa na mashabiki na wachezaji wenzake wa Yanga.
Mbali na hilo la kupigwa, Morrison amesema pia kitendo cha mkataba wake kumalizika, ndiyo kimechochea zaidi yeye kutoungana na wenzake mazoezini hadi sasa.

Morrison ambaye Julai 12, mwaka huu katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba, aliondoka uwanjani mara tu alipofanyiwa mabadiliko huku timu yake ikifungwa mabao 4-1.
Tangu siku hiyo, hajaungana na wenzake hadi leo huku akisema mkataba wake umemalizika Julai 15, mwaka huu. Nyota huyo raia wa Ghana, alijiunga na Yanga, Januari mwaka huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema: “Nimechoshwa kabisa na hali ya maisha ndani ya Yanga kwani mambo yanayoendelea kwangu na uongozi yanafanya hadi kutoelewana na nyota wenzangu.
“Nimesikia kuwa walipanga kunifanyia fujo mazoezini na ndiyo maana nikaona kwa kuwa mkataba wangu umemalizika ni bora nikae pembeni hadi pale nitakapopata muafaka wa madai yangu na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania),” alisema Morrison.
KIUNGO WA SIMBA ATIBUA DILI LA NYOTA WA RWANDA KUTUA YANGA MESSI AMPOTEZA MAZIMA BENZEMA WA REAL MADRID

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply