Uncategorized

HAWA HAPA NANE WA KIKOSI CHA KWANZA YANGA KUKOSA MTIBWA SUGAR LEO JAMHURI, DODOMA

admin July 21, 2020 9:47 pm


LEO Yanga inatupa kete ya 37 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo watamenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro majira ya saa 10:00 jioni.

Wachezaji wao nane wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ambazi zimeelezwa ikiwa ni pamoja  na wale ambao ni majeruhi pamoja na wale ambao hawapo kwenye mpango wa kocha.

Nyota hao ni pamoja na:-Haruna Niyonzima anasumbuliwa na majeraha ya goti, Mapinduzi Balama yeye pia anasumbuliwa na majeraha aliyopata mazoezini, Papy Tshishimbi bado hajawa fiti.

Ally Ally, Andrew Vincent, Eric Kabamba, Ramadhan Kabwili, Raphael Daud hawa hawapo kwenye mpango wa mwalimu, Luc Eymael hivyo iwapo atawatumia ni kwa muda mchache ndani ya kikosi cha leo.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 68 inamenyana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 41 zote zimecheza mechi 36.

MBELGIJI WA SIMBA AFICHUA SIRI ZA CHAMA NA SHEVA KAZI IMEANZA SIMBA, NYOTA SABA KUSEPA KIKOSINI MSIMU UJAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply