Uncategorized

MBELGIJI WA SIMBA AFICHUA SIRI ZA CHAMA NA SHEVA

admin July 21, 2020 9:47 pm

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa siri kubwa ya wachezaji wake kufanya vizuri kwenye mechi zao nyingi ni kutumia akili na utulivu mkubwa ndani ya uwanja.
Viungo wake wawili, Clatous Chama na Miraj Athuman,’Sheva’ wamekuwa na wakati mzuri kila wanapopata nafasi ya kuanza kucheza jambo ambalo linamfanya awe na uhakika wa kupata matokeo pindi wanapoanza.
Wawili hao wamehusika kwenye jumla ya mabao 19 kati ya 76 yaliyofungwa na Simba ambapo Chama amefunga mabao mawili na pasi 9 za mabao 2 huku Sheva akiwa amefunga mabao 7 na asisti  moja.
Sven amesema kuwa :-“Kila mchezaji ndani ya timu ni muhimu na wote wana nafasi zao katika kuzitimiza, huwa ninashindwa kuwatumia wote kwa kuwa nina wachezaji wengi na kanuni haziruhusu hayo yatokee, ila ukimzungumzia Chama, Miraj wanatumia akili na utulivu mkubwa wakiwa ndani ya uwanja.
“Huwa ninawaambia mara kwa mara kuwa wawapo uwanjani wanapaswa wafikirie jambo moja ambalo ni ushindi na hautaweza kupata ushindi ikiwa hautatulia katika kufanya maamuzi na kutumia akili hivyo hicho ni kitu cha kuzingatia pamoja na juhudi mazoezini.”

MASHINE HIZI ZA KAZI ZIMEANDALIWA NA YANGA KUIMALIZA MTIBWA SUGAR LEO HAWA HAPA NANE WA KIKOSI CHA KWANZA YANGA KUKOSA MTIBWA SUGAR LEO JAMHURI, DODOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply