Uncategorized

MASHINE HIZI ZA KAZI ZIMEANDALIWA NA YANGA KUIMALIZA MTIBWA SUGAR LEO

admin July 21, 2020 9:47 pm


NYOTA wawili wa Yanga, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ na Mrisho Ngassa wameandaliwa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakachoezwa leo, Julai 22, Uwanja wa Jamhuri.
Yanga ilitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC, mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa ambapo bao pekee kwa Yanga lilifungwa na kiungo, Fei Toto akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa wachezaji wake jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mechi zake zijazo ikiwa ni dhidi ya Lipuli.
β€œWachezaji wangu wote wapo vizuri na bado tunapambania malengo yetu ya kumaliza ligi tukiwa nafasi ya pili hilo ili liwezekana tunahitaji kushinda mechi zetu zilizopo mbele yetu.
β€œKila mchezaji yupo tayari kuanzia Ngassa, Fei, Abdul (Juma) hivyo ni jambo la kusubiri kuona namna gani kazi inaweza kukamilika ndani ya uwanja, mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema Eymael.
Yanga inakutana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya KMC ikiwa inapambana kujinasua kushuka daraja huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 68 zote zimecheza mechi 36.
SIMBA WATIA TIMU TANGA, ALHAMISI KUVAANA NA COASTAL UNION MBELGIJI WA SIMBA AFICHUA SIRI ZA CHAMA NA SHEVA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply