GHAFLA tu Mtibwa Sugar imeanza kuporomoka kwenye ramani ya soka Bongo huku ikiwa ina kila kitu kinachoitwa vipaji pamoja na miundombinu.
1988 ilianzishwa na kundi la wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi kwenye kiwanda hicho kupitia sekta ya michezo na kucheza kwa pamoja ndani ya kiwanda hicho kilichopo Morogoro ikaundwa Mtibwa Sugar.
1995 kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Klabu hiyo Thobias Kifaru ilianza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na haijawahi kushuka na kwa misimu 10 mfululizo ilikuwa kawaida kumaliza ikiwa ndani ya 10 bora.
Mataji mawili ya Kombe la Ligi Kuu Bara ilitwaa 1999 na 2000 chini ya Kocha Mkuu, Jonas Mkoko na alimfundisha Zuber Katwila ambaye ni Kocha Mkuu wa sasa ndani ya kosi hilo.
Taji moja la Kombe la Shirikisho ililitwaa 2018 iliposhinda mabao 2-1 mbele ya Singida United, Kombe la Mapinduzi mataji mawili, 2000 na 2019 ilipoitungua Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.
Mtibwa Sugar ina uwanja wao na hosteli kwa ajili ya wachezaji zilizopo mkoani Morogoro. Uwanja wao unaitwa Manungu.Uwanja wao wanaoutumia kwenye mechi za Ligi Kuu Bara kwa sasa ni Gairo kwa mechi zisizo na mashabiki wengi ila zile za Simba na Yanga ni Uwanja wa Jamhuri.
Ndani ya misimu 10 iliweza kuleta ushindani kwenye ligi na kuwa miongoni mwa timu ambazo zinafanya vizuri ndani ya Bongo.
Ndani ya tano bora
Nafasi ya nne ilikuwa ni nafasi ya juu kwa Mtibwa Sugar ndani ya misimu 10 mfululizo ambapo msimu wa 2010/11 ikiwa na pointi 36 na msimu wa 2011/12 ilimaliza ikiwa nafasi ya nne na pointi zake 42.
2012/13, ilimaliza ikiwa nafasi ya tano ikiwa na pointi
39 na msimu wa 2015/16 ilimaliza ikiwa nafasi ya tano na pointi 50. 2016,/17 nafasi ya 5 ikiwa na pointi 44 na 2018/19 nafasi ya 5 ikiwa na pointi 50. Ndani ya 10 bora
2017/18 nafasi ya 6 ikiwa na pointi 41
2013/14 ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya 7 na pointi 31. 2014/15 nafasi ya 7 ikiwa na pointi 31. Kuboronga Msimu wa 2019/20 mambo yamekuwa magumu kwa Mtibwa Sugar ambapo bado hawana uhakika wa kumaliza ndani ya 10 bora kwa sasa kutokana na mwendo wao wa kusuasua. Ikiwa imecheza mechi 36 baada ya kumenyana na KMC ilikuwa imeshinda mechi 10, sare 11, kupoteza 15 na kujiwekea kibindoni pointi 41 ipo nafasi ya 14.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ni kipindi cha mpito wanachopitia ila wana imani ya kubaki ndani ya ligi.
“Tupo kwenye kipindi cha mpito ambacho tunapitia kabla ya janga la Virusi vya Corona tulikuwa tunaanza kurejea kwenye ubora wetu ila ilivyotokea mambo yakawa magumu kwetu.
“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu ambazo zimebaki tutapata ushindi na hatutashuka,” alisema.
Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar alisema kuwa kupoteza kwao kwenye mechi ndani ya uwanja ni makosa ambayo yanafanywa ndani ya uwanja.
“Kila baada ya mchezo tumekuwa tukifanya tathimini na kuangalia pale ambapo tunakosea ili tusifanye makosa bado tunapambana ili kurejea kwenye ubora wetu kwa kuwa uwezo tunao,” alisema Katwila.
Msimu huu timu nne zinashuka jumlajumla, Singida United washajiengua zimebaki timu tatu ambazo zitashuka.
|
|
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.