Home Uncategorized SIMBA YAIKIMBIZA YANGA,AZAM FC NDANI YA BONGO

SIMBA YAIKIMBIZA YANGA,AZAM FC NDANI YA BONGO


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweza kukiongoza kikosi chake kuweka rekodi za kibabe ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwakimbiza wapinzani wake wote 19 ndani ya ligi.
Ikiwa imetwaa ubingwa mapema ikiwa imebakiza mechi sita mkononi kwa sasa ina mechi mbili baada ya kucheza mechi 36 ina pointi 84 kibindoni inaweza kumaliza ikiwa na pointi 90 kama itashinda mechi zake mbili zilizobaki, leo itamenyana na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani Tanga na itamalizana na Polisi Tanzania zote ugenini.
Kwa upande wa mabao ya kufunga, Simba inakimbiza ikiwa na mabao  76 ya kufunga huku ikiwa  imefungwa mabao 20 ambayo ni machache ndani ya dakika 3,240 ilizotumia uwanjani ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 72 na ikiokota nyavuni bao kila baada ya dakika 162.
Mbali na kuwa vinara kwa kutupia mabao pia kinara wa utupiaji ndani ya ligi ni Meddie Kagere mwenye mabao 22 anafuatiwa kwa ukaribu na mzawa Yusuph Mhilu anayekipiga Kagera Sugar  ana mabao 13. Mtengeneza mipango namba moja ndani ya ligi ni Clatous Chama mwenye pasi 9 na ana mabao mawili kibindoni.
Yanga imewashika shati Simba kwenye upande wa mechi za kupoteza ambapo wote wamepoteza jumla ya mechi nne. Simba imenyooshwa na Mwadui FC, JKT Tanzania, Yanga na Mbao FC. Yanga wenyewe wamenyooshwa na Ruvu Shooting, Azam FC, Kagera Sugar na KMC
Mshindani wake wa karibu kwa upande wa safu ya ushambuliaji ni Azam FC, imefunga jumla ya mabao 49 pia na kwa upande wa safu kali ya ulinzi Azam wapo nafasi ya pili imefungwa jumla ya mabao 24.
SOMA NA HII  CORONA YAMFANYA MORIS KUMKUBUKA KOCHA