Uncategorized

JUMA MGUNDA AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE

admin July 24, 2020 2:47 pm


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa vijana wake wamekuwa na morali kubwa ya kupambana ndani ya uwanja kwa kuwa wanatimiza wajibu wao.

 Mgunda jana, Julai 23 alikiongoza kikosi chake kwenye sare ya bila kufungana na mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo ngome zote zilikuwa ngumu ndani ya dakika 90 huku Simba ikikamilisha dakika 90 bila beki wao kisiki, Pascal Wawa ambaye alionyeshwa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu.

Mgunda amesema:”Vijana wangu wanajua wajibu wao na wanajituma hivyo kupata sare kwenye mchezo wetu ni jambo la kushukuru kwani mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, nawapongeza vijana.”

Mchezo wake unaofuata ambao ni wa mwisho kwa mzunguko wa pili msimu wa 2019/20 utakuwa Julai 26 dhidi ya JKT Tanzania.

BREAKING:PREMIER LEAGUE KUANZA SEPTEMBA 12 BREAKING:MECHI ZA LIGI KUU BARA KUPANGIWA TAREHE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply