Uncategorized

SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MEZEMBE, KUCHOMOKA NA BEKI MMOJA

admin July 25, 2020 9:47 pm

KLABU ya Simba imedhamiria kusajili kikosi cha kimataifa baada ya kuwa katika mchakato wa kusajili beki kutoka Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo imejihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao ambapo uongozi wa timu hiyo tayari umeshaweka wazi kutaka kufanya usajili kabambe wa wachezaji wa kimataifa ili kuleta ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Meneja wa mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, Patrick Gakumba amesema kuwa, kuna mazungumzo kati yake na uongozi wa Simba juu ya kushusha beki kutoka TP Mazembe ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
“Nipo katika mazungumzo na viongozi wa Simba juu ya kuwaletea beki mwenye kiwango cha juu ambapo tayari nimeshampata beki huyo anayekipiga katika Klabu ya TP Mazembe japokuwa siwezi kumtaja kwa sasa ni nani kwa kuwa sheria inanikataza kumtaja mchezaji akiwa bado hajasaini.
“Mipango ikikamilika Simba watamsajili beki kutoka TP Mazembe ambaye ana uzoefu mzuri katika mashindano ya kimataifa kwani timu yake hiyo imeshawahi kufika fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Mazungumzo yanakwenda vizuri kati yangu na uongozi wa Simba na mambo yakikaa sawa basi nitamuweka wazi mchezaji huyo na dau watakalotumia kumsajili,” alisema Gakumba.

Chanzo:Championi
UNAI EMERY APATA SHAVU LA MIAKA MITATU BAADA YA KUKAA BILA KAZI TANGU NOVEMBA YANGA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU TSHISHIMBI, NIYONZIMA BADO UTATA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply