Uncategorized

JEMBE JIPYA SIMBA KUTOKA GHANA KILA KITU FRESH

admin July 27, 2020 9:47 pm

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Rayon Sports, Michael Sarpong, amefunguka kuwa kwa sasa anasubiria viongozi wa Simba wamtumie tiketi ili aweze kutua kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
Sarpong, raia wa Ghana, inaelezwa amemalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ambayo iliamua kumtema kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu.
Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu, ameliambia Championi Jumatatu kuwa kila kitu upande wake kipo sawa na kwa sasa wanasubiria simu kutoka kwa viongozi wa Simba ili waje kukamilisha dili la kujiunga na timu hiyo.
“Kila kitu kipo sawa, nadhani sasa hivi imebakia kwa upande wa Simba wao ndiyo wanajua lini naweza kuja huko na meneja wangu kwa ajili ya kusaini mkataba.
“Lakini naamini halitakuwa suala la kuchelewa sana kwa sababu nimeambiwa wataanza maandalizi ya msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa hivyo matarajio yangu mapema mwezi ujao nitakuwa huko,” alisema Sarpong.
DUH! KOSI LA WATUKUTU LIGI KUU BARA, SIMBA YANGA ZAFUNIKA MATOLA WA SIMBA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply