Uncategorized

SABA WA SIMBA KUIKOSA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO DHIDI YA NAMUNGO

admin July 29, 2020 9:47 pm


AGOSTI 2, Uwanja wa Nelson Mandela Simba inatarajiwa kuchezwa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kupambania taji hilo muhimu.

Tayari Simba ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara hivyo iwapo watafanikiwa kulitwaa taji hilo watabeba kombe huku nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ikiwa mikononi mwa mshindi wa pili ambaye ni Namungo.

Ikiwa Namungo itashinda, itatwaa taji na kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa meneja wa Simba. Patrick Rweyemamu amesema kuwa kikosi ambacho kilikwenda Tanga kucheza na Coastal Union kisha kikamalizana na Polisi Tanzania kule Moshi ndicho ambacho kinaelekea Sumbawanga.

“Wachezaji wote wapo vizuri na wanaendelea salama, wale ambao tulikuwa nao Moshi na Tanga ndio ambao tupo, ” amesema.

Wachezaji ambao walikosa michezo hiyo miwili na inatarajiwa watakosa fainali ni hawa hapa saba ikiwa ni pamoja na:-Ibrahim Ajib, Sharaf Shiboub, Rashid Juma, Haruna Shamte, Shiza Kichuya, Cyprian Kipenye na Tairone Santos.

MBAO YAANZA KWA KUCHECHEMEA PLAY OFFS YANGA YAPIGWA BAO NA SIMBA KWA MTUPIAJI HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply