Uncategorized

PLUIJM: NIPO TAYARI KUREJEA KUIFUNDISHA YANGA

admin July 30, 2020 10:47 am

KOCHA wa zamani wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm ameibuka na kufungukia hatma yake ya kurejea kukinoa kikosi baada ya tetesi nyingi kuzagaa anakuja tena kwa mara ya tatu kuifundisha timu hiyo.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo jina lake litajwe kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na Yanga baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbelgiji, Luc Eymael kufutwa kazi.
Kocha mwingine anayetajwa ni Ernie Brandts naye raia wa Uholanzi ambaye jina lake linatajwa kwenye orodha ya makocha wanaotarajiwa kujiunga na Yanga katika msimu ujao.
Pluijm amesema kuwa bado viongozi wa Yanga hawajamfuata kwa ajili ya kufanya mazungumzo, lakini yeye yupo tayari kurejea kukinoa kikosi hicho kama watahitaji huduma yake katika msimu ujao.

Pluijum amesema kuwa hivi sasa amewaachia viongozi wa Yanga ambao ndiyo watakaochukua maamuzi ya yeye kuja au kutokuja kukinoa kikosi hicho.
“Mashabiki wa Yanga wanaonekana kukumbuka falsafa yangu ya uchezaji wa soka, hiyo ndiyo maana nimekuwa nikipokea meseji nyingi za kuniomba nirejee tena kuifundisha Yanga.
“Kwangu ngumu kusema ninakuja kuifundisha Yanga, kwani hayo ni maamuzi ya uongozi ambao kama utakuwa tayari kunirejesha, basi nitakuwa tayari kurejea tena.
“Kwa hivi sasa sina timu yoyote ninayoifundisha, hivyo kikubwa ni viongozi kunifuata na kufanya mazungumzo na mimi, kama tukifikia muafaka mzuri basi nitakuwa tayari kurudi, uzuri nawafahamu wachezaji baadhi ambao bado wapo niliwahi kufanya nao kazi, hivyo sitakuwa na kazi kubwa,”alisema Pluijm.
AGOSTI 14 MLIMANI CITY, BONDIA WA NGUMI KAONEKA ATAMBA KUWA AKIPIGWA NA KIDUNDA ANAACHA NGUMI SHOO YA MZEE YUSUF ILIYOPANGWA KUFANYIKA JULAI 7 SASA ITAKUWA NI SIKU YA MKESHA WA NANENANE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply