Uncategorized

GWAMBINA FC MAMBO YAMEANZA, LEO KUANZA KUFANYA MAJARIBIO KWA WACHEZAJI

admin August 4, 2020 9:47 am


UONGOZI wa Gwambina FC leo Agosti 4 unaanza kufanya majaribio kwa wachezaji wanaohitaji kucheza ndani ya kikosi hicho.

Gwambina FC ina uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 baada ya kukata tiketi hiyo kwa kuwa vinara ndani ya Ligi Daraja la Kwanza kundi B.

Ipo nafasi ya kwanza na pointi 47 baada ya kucheza mechi 22 ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.

Zoezi hilo linaanza leo chini ya Kocha Mkuu, Novatus Fulgence na majaribio hayo yatadumu mpaka Agosti 11.

Wachezaji wanatakiwa kujigharamia kila kitu kuanzia malazi na chakula kwa siku zote watakazokuwa hapo Mwanza.

Pia kwa wachezaji wanaohitaji kucheza kwenye timu ya vijana chini ya miaka 20 lazima waende na vyeti vya kuzaliwa ili kuthibitisha miaka yao. 

KIPA NAMBA MBILI WA SIMBA, BENO KAKOLANYA ATAJWA KUIBUKIA AZAM FC NYOTA WATATU WA YANGA WAKOMBA MILIONI 210, MTUPIAJI NAMBA MOJA WA MBAO AKAMILISHA IDADI YA MAJEMBE MANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply