Uncategorized

SUALA LA MORRISON KUIBUKIA SIMBA PICHA BADO LINAENDELEA

admin August 9, 2020 10:47 am

 

BAADA ya Simba kumtangaza Bernard Morrison kuibukia ndani ya kikosi cha Simba akitokea Yanga, tayari jambo jingine limeibuka baada ya Shirikisho la soka Tanzania, (TFF) kuwaita Yanga kesho makao makuu kuhusu suala hilo.


Morrison yupo kwenye mvutano mkubwa na Yanga hasa kwenye suala la mkataba ambapo yeye alisema kuwa mkataba wake ulikuwa wa miezi sita huku Yanga wakisema kuwa ana dili la miaka miwili.


Jana, Agosti 8, Simba ilimtambulisha Morrison ndani ya Simba jambo ambalo limevuta mvutano ambapo Yanga ilitoa taarifa kwamba inalifuatilia suala hilo ili kuweza kuchukua hatua.


Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa kesho TFF itatoa hukumu ya kesi ambayo ilifunguliwa na Yanga kuhusu mkataba wa Morrison wa miaka miwili na hatma yake kuibukia Simba itajulikana.

PIRLO ARITHI MIKOBA YA SARRI KWA MIAKA MIWILI JUVENTUS NYOTA MPYA YANGA ATAKA KUFUNGA MABAO ZAIDI YA 30

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply