Uncategorized

NYOTA MPYA YANGA ATAKA KUFUNGA MABAO ZAIDI YA 30

admin August 9, 2020 12:47 pm

 WAZIR Junior, nyota mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anahitaji kufunga mabao zaidi ya 30 kwa msimu wa 2020/21.

Junior amejiunga na Yanga akitokea Klabu ya Mbao iliyokuwa inanolewa na Felix Minziro ila msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa ilitolewa na Ihefu kwenye mchezo wa playoffs uliochezwa Uwanja wa Kirumba, ambayo ilipenya kwa faida ya mabao ya ugenini.

Akiwa Mbao FC alifunga mabao 15 ambapo kwenye ligi alifunga 13 na kwenye mchezo wa Playofs alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-2 ila mchezo wa kwanza walichapwa mabao 2-0 walipocheza na Ihefu, Mbeya.


“Ninapenda kufunga kwa kuwa ni kazi yangu na ndugu zangu na jamaa zangu wengi ni mashabiki wa Yanga hivyo nitafurahi nikifunga mabao zaidi ya 30 ndani ya msimu mpya,” amesema.

SUALA LA MORRISON KUIBUKIA SIMBA PICHA BADO LINAENDELEA DEO KANDA ATAJWA KUIBUKIA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply