Uncategorized

BWALYA WAHUSISHWA KUIBUKIA YANGA NA SIMBA

admin August 15, 2020 10:47 am


INAELEZWA kuwa  Larry Bwalya na Walter Bwalya wote raia wa Zambia wapo kwenye rada za kuibukia ndani Simba na Yanga.
Larry Bwalya  mwenye miaka 25 yeye ni kiungo mshambuliaji anakipigandani ya Ligi Kuu ya Zambia kwenye Klabu ya Power Dynamos anahusishwa kujiunga na Yanga na inaelezwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaendelea vizuri.

👉Walter Bwalya  mwenye miaka 25 huyu ni mshambuliaji wa zamani wa Nkana FC (The Red Devils) kwa sasa anakipiga Ligi Kuu ya Misri kwenye Klabu ya El Gouna FC yeye anahusishwa kujiunga na Simba.


Kwa muda mrefu Bwalya amekuwa akitajwa kuibukia Simba ila kikazwo awali ilikuwa inatajwa kuwa ilikuwa ni dau kubwa ila kwa sasa mambo yanaelezwa kuwa safi kwa pande zote mbili kuelewana.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wapo vizuri katika masuala ya usajili wana imani ya kuwa na kikosi bora cha ushindani.

 
BREAKING:KIGOGO YANGA APIGWA CHINI MAZIMA DAVID KAMETA MAARUFU KAMA DUCHU ATUA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply