Uncategorized

MUANGOLA HUYU AINGIA ANGA ZA YANGA

admin August 18, 2020 1:47 pm

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga iko kwenye hatua za mwisho za  kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Interclube ya Angola, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes ‘ Carlinhos’ raia wa Angola.


Hiyo ni siku chacha baada ya kukamilisha dili la nyota wawili wa kimataifa kujiunga na timu hiyo kwa dili la miaka miwili ambao ni Tuisila Kisinda ambaye ni kiungo pamoja na Tonombe Mukoko ambaye yeye ni mshambuliaji.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa bado kuna nyota wengine wa kimataifa wanafanya nao mazungumzo hivyo mipango ikamilika wataweka kila kitu wazi.

“Kuna nyota mwingine raia wa Angola tupo naye kwenye mazungumzo ya mwisho, mambo yakikamilika basi kila kitu kitawekwa wazi,” amesema.
SIMBA DAY AGOSTI 22 NI DHIDI YA TIMU YA BURUNDI,MAJEMBE HAYA KUTAMBULISHWA MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI KUU BARA KUPIGWA AGOSTI 30

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply