Uncategorized

MAXIME HAUZWI AENDELEA KUKINOA KIKOSI CHA KAGERA SUGAR, MECHI ZAKE HIZI HAPA

admin August 21, 2020 10:47 am

 


MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ndani ya msimu wa 2020/21 mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya JKT Tanzania,utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.

Maxime alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Yanga ili kuvaa mikoba ya Luc Eymael ambaye alifutwa kazi Julai 27 bado atazidi kuwa ndani ya kikosi hicho baada ya uongozi wa timu hiyo kusema kuwa hauzwi.

Akimalizana na JKT Tanzania, Septemba 7 atakutana na Gwambina FC, Septemba 11 atakuwa ugenini kisha kazi yake nyingine itakuwa mbele ya Yanga, Septemba 19 Uwanja wa Kaitaba.

Atamaliza mwezi Septemba akiwa Kaitaba kwa kumenyana na  Klabu ya KCM, Septemba 25.

Tayari kwa sasa Kagera Sugar wameanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine watakayoshiriki ndani ya msimu wa 2020/21.

HAJI AWAPA TANO YANGA, AWACHOKONOA ISHU YA KUMBEBA KIONGOZI JUU SIMBA YAAGIZA GPS ZA WACHEZAJI, LENGO KUWAFUATILIA KILA HATUA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply