Uncategorized

KOCHA MPYA BARCA AWAFUNGULIA MLANGO SUAREZ, BUSQUETS, JORDI ALBA

admin August 23, 2020 8:47 am

 

IMERIPOTIWA kuwa, kocha mpya wa Barcelona, Ronald Koeman, amewafungulia njia ya kutokea mastaa watatu wakubwa wa timu hiyo ambao ni Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba.

 

Koeman ametua Barca hivi karibuni akitokea timu ya Taifa ya Uholanzi akichukua nafasi ya Quique Setien.

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, kwa sasa anajipanga kupata timu ya ushindani huku akisema kuna baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza hawapaswi kuguswa katika mpango wa kuondolewa.

Wachezaji hao ni pamoja Lionel Messi, Marc-Andre ter Stegen. Frenkie de Jong, Clement Lenglet na Nelson Semedo, huku Antoine Griezmann na Ousmane Dembele wakipewa nafasi nyingine ya kuonyesha ubora wao.

Imeelezwa kuwa Koeman pia anataka kuendelea kufanya kazi na beki mkongwe wa timu hiyo, Gerard Pique kwani ni mhimili mkubwa kwenye ulinzi.

ILE ISHU YA RUSHWA INAYOMKABILI MAGUIRE NCHINI UGIRIKI SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply