Home Uncategorized MUANGOLA WA YANGA NA MORRISON WA SIMBA WALIPA MILIONI 36 TFF

MUANGOLA WA YANGA NA MORRISON WA SIMBA WALIPA MILIONI 36 TFF

 


KLABU kongwe za Simba na Yanga, zimelazimika kulilipa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kiasi cha shilingi milioni 36 kwa pamoja ikiwa ni ada ya malipo ya wachezaji wake wa kigeni waliowasajili hadi sasa katika msimu ujao.

 

Simba imesajili wachezaji wapya wa kigeni wanne katika dirisha linaloendelea hivi sasa ambapo kila mchezaji wanamlipia ada ya shilingi milioni nne ambayo ni sawa na shilingi milioni 16 kwa jumla ya wachezaji wanne/


Kwa upande wa Yanga yenyewe imesajili wachezaji watano wa kigeni hadi sasa katika usajili unaoendelea ambapo kila mchezaji analipiwa ada ya milioni nne ikiwa ni sawa na milioni 20 ambapo ukizijumlisha kwa pamoja Simba na Yanga wanalipa milioni 36 kwa ajili ya ada za wachezaji wa kigeni waliowasajili.




 

Huu ni utaratibu ambao umewekwa na TFF ili kuhakikisha kila mchezaji wa kigeni anayetua katika timu yeyote ya ligi kuu lazima alipiwe ada hiyo ndipo usajili wake uweze kukamilika na kuruhusiwa kucheza ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya kazi na makazi.

 

Simba imewasajili wachezaji; Bernard Morrison aliyetokea Yanga kwa dau la shilingi milioni 230, Chris Mugalu (Sh 140), Larry Bwalya (Sh 138) na Joash Onyango (Sh 80).


Yanga imemsajili Tuisila Kisinda kwa Sh 230, Mukoko Tonombe (Sh 230) ambao wote wamesajiliwa wakitokea AS Vita ya DR Congo, Michael Sarpong (Sh 120) raia wa Ghana aliyetokea Rayon Sports ya Rwanda, Yacouba Sogne (Sh 100) raia wa Bukina Faso akitokea Klabu ya Asante Kotoko ya Ghana na Carlos Stenio ‘Carlinhos’ kutoka Angola.

 

Simba na Yanga zipo katika mbio za kuusaka ubingwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2020/21 ambapo kila upande umeonyesha kujiimarisha katika usajili ili kuleta ushindani.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA MWADUI FC, KUSUKA KIKOSI KIPYA CHA KUTISHA