Uncategorized
JEMBE LA KAZI YANGA KUTOKA BURKINA FASO LATIA TIMU BONGO RASMI
YACOUBA Sogne mshambuliaji wa Yanga amewasili Tanzania leo Agosti 31 akitokea nchini Burkina Faso.
Sogne anaungana na wachezaji wenzake kambini jumla kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.
Yanga itaanza na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Septemba 6, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Sogne ambaye amesaini dili la miaka miwili amesema kuwa anafurahi kuwa sehemu ya timu na anafurahi kwa mapokezi.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.