Uncategorized

KOCHA ARSENAL AFUNGUKIA SAINI YA AUBAMEYANG

admin September 3, 2020 4:47 am

 

MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa mshambuliaji wake namba moja Pierre Emerick Aubameyang atasaini dili jipya hivi karibuni. 

Arteta ameongoza kikosi chake kutwaa mataji mawili kwa kuzinyoosha timu kubwa ikiwa ni pamoja na ule wa Kombe la FA ambapo aliichapa Chelsea mabao 2-1 na taji la Ngao ya Jamii alishinda kwa penalti 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1.

Mtupiaji wa mabao yote matatu alikuwa ni nahodha Aubameyang ambaye amekuwa akitajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Arteta amesema:”Nimekuwa nikisema jambo lilelile kuhusu Aubameyang. Ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza michezo mikubwa.

“Nimekuwa nikipambana kuhakikisha namshawishi ili aweze kubaki kwenye timu hii naamini kuwa atakubali kusaini kwa kuwa hii ni timu yake bora na tukiwa pamoja tutafanya makubwa msimu ujao,”.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12 na mabingwa watetezi ni Liverpool.

MUONEKANO WA KAMBI MPYA YA YANGA 2020/21 MSERBIA AANZA NA WAWILI YANGA,SVEN APIGA MKWARA, NDANI YA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply