Uncategorized

AZAM FC WAKIWASHA VPL,WAICHAPA BAO 1-0 POLISI TANZANIA

admin September 7, 2020 6:47 pm

 KIKOSI cha Azam FC leo Septemba 7 kimefungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania. 

Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa uliwafanya matajiri wa Dar es Salaam kusubiri mpaka dakika ya 44 kupachika bao la ushindi.

Bao hilo lilipachikwa na mshambuliaji namba moja wa Azam FC, Obrey Chirwa kwa pasi ya Prince Dube.

Jitihada za Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini kupambana kuweka usawa ziligonga mwamba mbele ya beki bora wa msimu uliopita, Nocolas Wadada.

Azam inayonolewa na Aristica Cioaba inazibakiza pointi zote tatu Chamazi. Inaanza kujiaanda dhidi ya Coastal Union, Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex.

MTIBWA SUGAR V SIMBA, NI VITA NDANI YA UWANJA WAJEDA WASEPA NA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR KAITABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply