Uncategorized

WAJEDA WASEPA NA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR KAITABA

admin September 7, 2020 6:47 pm

 

KAGERA Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Mexime leo, Septemba 7, imeanza kwa kupokea kichapo mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo umechezwa,  Uwanja wa Kaitaba na kuwafanya mashabiki wa Kagera Sugar kushuhudia timu hiyo ikifungwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi kwa JKT Tanzania lilipachikwa kimiani na mshambuliaji wa timu hiyo, Adam Adam.

Bao hilo lililopachikwa dakika ya 16 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya Kagera Sugar kuyeyusha pointi tatu za mwanzo mazima.

Baada ya mchezo wa leo wanaanza kujiaandaa na mchezo dhidi ya Gwambina FC utakaopigwa Septemba 11. Inakutana na Gwambina FC ambayo nayo imetoka kunyooshwa kwa bao 1-0 mbele ya Biashara United ya Mara.

AZAM FC WAKIWASHA VPL,WAICHAPA BAO 1-0 POLISI TANZANIA MZUNGUKO WA KWANZA VPL NOMA,MABAO 14 YAFUNGWA,KMC BABA LAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply