Home Uncategorized YANGA WATAJA SABABU ITAKAYOWAPA UBINGWA

YANGA WATAJA SABABU ITAKAYOWAPA UBINGWA


 KIUNGO wa Yanga,  Haruna Niyonzima, amesema kuwa wana kila sababu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa wana kikosi bora.

 

Niyonzima ambaye msimu uliopita akiwa na Yanga aliweza kutimiza majukumu yake vema kabla ya kupata majeraha kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United aliweza kufunga mabao mawili ambapo moja alifunga kwenye ligi na moja alifunga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.


Baadhi ya waliosajiliwa na Yanga ni Michael Saprong, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Faridi Mussa, Yacouba Songne, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior na Kibwana Shomari.


 Niyonzima amesema kuwa kati ya vitu ambavyo wamevifanya uongozi wa timu hiyo ni usajili ulio bora kwenye wachezaji wa viwango tofauti na msimu uliopita.

 

Niyonzima amesema kuwa usajili huo bora utaongeza hali ya ushindani wa namba katika timu kutokana na kila mmoja kuwepo kwenye kiwango kizuri katika kuhakikisha wanapata matokeo.

 

Aliongeza kuwa katika msimu uliopita, timu yao ilikuwa na upungufu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo anaamini ndiyo ilisababaisha waukose ubingwa wa ligi.


“Msimu huu lazima uwe wetu Yanga, hiyo ni kutokana na usajili bora uliofanyika hasa katika safu ya ushambuliaji ambayo ndiyo ilisababisha tuukose ubingwa.


“Kama safu ya ushambuliaji ingekuwa bora, basi tungechukua ubingwa msimu uliopita, kwani washambuliaji wetu walikuwa wanapata nafasi nyingi za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia.

 

“Lakini ujio wa washambuliaji wapya utaiwezesha timu kupata matokeo mazuri ya ushindi, kikubwa viungo tunatakiwa kutengeneza na kutumia nafasi zote tunazozipata kuhakikisha tunazitumia vema kwa kufunga mabao,” amesema Niyonzima.


Chanzo:Championi.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA KUTUA BONGO LEO