Uncategorized

YANGA: TUMEWEKA REKODI YA KIPEKEE, WAPIGAJI DAWA YAO IPO

admin September 11, 2020 12:47 pm

 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umeweza kuweka rekodi ya kuzindua jezi mpya pamoja na duka la vifaa ndani ya makao makuu ya timu hiyo yaliyopo mtaa wa Jangwani, Kariakoo.


Leo Septemba 11, Yanga imezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21 na mashabiki wengi pamoja na wadau walijitokeza kushuhudia uzinduzi huo na kuanza kununua jezi hizo.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kwa wale ambao watachakachua jezi hizo watakuwa matatani kwa kuwa wanashirikiana na mamlaka ya dola pamoja na mtandao mkubwa wa kufanya uchunguzi tofauti na msimu uliopita.


Mwakalebela amesema:”Tumekuwa timu ya kwanza kuzindua duka la vifaa vya Yanga pamoja na jezi nzuri na yenye ubora hivyo tupo imara katika kila idara na tunaamini kwamba tutafanya mengi makubwa.


“Mashabiki wametushangaza kwa kununua na kuzivaa jezi wakati huu tofauti na msimu uliopita na hii inamaanisha kwamba mashabiki wanaipenda timu na wanawekeza ndani ya timu na tunampango wa kusambaza jezi kwenye maduka mengine.”

SHIBOUB AKUNJA MKWANJA WA MAANA KWA WAARABU ISHU YA BILIONI 20 ZA MO NA KINGWANGALLA IMEFIKIA HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply