Uncategorized

RAIS LA LIGA: ILIKUWA NGUMU KUMUACHIA MESSI

admin September 13, 2020 8:47 am

 


RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, Javier Tebas, amesema kuwa kwao ilikuwa ni ngumu kumuachia mchezaji staa wa ligi hiyo, Lionel Messi aondoke.

 

Messi alishatangaza kuondoka kwenye ligi hiyo na kwenda Manchester City, lakini ghafla alibadilisha mawazo na kuamua kubaki kwenye timu hiyo baada ya majadiliano marefu na klabu yake.

 

Messi aligoma kufanya mazoezi kwa wiki nzima na Barcelona na kwa sasa baada ya kusitisha mpango wake wa kutaka kusepa ameanza mazoezi na wachezaji wenzake.


Rais huyo amesema alipambana mwenyewe kuhakikisha kuwa mshambuliaji huyo bora duniani anabaki kwenye ligi hiyo.

 

Wakati Messi akisema kuwa anaondoka bure, La Liga walitoa taarifa iliyokuwa ikionyesha kuwa ili kumpata mchezaji huyo unatakiwa kutoa kitita cha pauni milioni 630, sawa na shilingi trilioni 2.

 

“Kama ligi lazima tulinde sheria na kufuata haki, kila mchezaji lazima aheshimu mkataba wake.


“Ukweli mimi sikuona mpambano kati ya Messi na klabu yake, kwanza natakiwa kumheshimu sana kwenye hilo na jinsi alivyokaa kwenye ligi hii kwa muda mrefu.

 

“Namheshimu sana Messi, nampenda sana na historia aliyotengeneza hapa kwa miaka 20 inajionyesha.Nafikiri suala langu lilikuwa kuwa mkataba unaoheshimiwa, lakini vizuri pia ni kwamba walikaa wenyewe na kukubaliana na yote yakaisha, lakini kwangu ilikuwa mgumu kumuona anaondoka kwenye La Liga,” amesema rais huyo.

 

SABABU YA MUANGOLA WA YANGA KUJENGA USHKAJI NA BENCHI HII HAPA ISHU YA JEZI, YANGA YAIPIGA DONGO KIMTINDO SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply