Yanga vs Gaborone United
Yanga SC

Mngqithi Atoa Onyo Zito: Yanga Yaiva Kuikabili Gaborone United Ligi ya Mabingwa Afrika!

Vardo September 4, 2026 5:40 pm

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amesisitiza kuwa kikosi chake kipo katika hali nzuri na kimejipanga kikamilifu kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho, Jumamosi, kwenye Uwanja wa Taifa wa Gaborone nchini Botswana, katika mchezo ambao utaweka mwelekeo wa safari yao ya kimataifa msimu huu.

Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, Mngqithi alieleza kuwa licha ya ugumu wa ratiba yenye michezo miwili mfurulizo, benchi la ufundi limetumia vizuri siku chache walizopata kukaa na wachezaji ili kuweka mbinu sawa.

“Tunaenda kucheza mchezo muhimu sana kwetu. Mwishoni mwa wiki hii tuna michezo miwili, lakini kwa bahati nzuri tumepata muda wa kutosha wa kujiandaa na kikosi na tuko tayari kwa mapambano,” alisema Mngqithi.

Mheshimu Mpinzani: Mbali na maandalizi ya kikosi chake, Mngqithi alitumia fursa hiyo kumwagia sifa Kocha Mkuu wa Gaborone United, Sean Connor, kwa kazi kubwa aliyoifanya kuijenga timu hiyo kuwa ya ushindani mkubwa.

“Lazima nimpe heshima yake Kocha Sean Connor. Amefanya kazi kubwa mno. Tangu anaanza kuifundisha Gaborone United nimekuwa nikiifuatilia kwa karibu, na kwa hakika ameibadilisha na kuwa timu hatari sana,” aliongeza Mngqithi.

Kauli hii ya Mngqithi inaonyesha kuwa Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanaiingia mechi hiyo kwa umakini mkubwa bila kuwadharau wapinzani wao. Matokeo mazuri ugenini yatawapa Yanga faida kubwa kabla ya kuwakaribisha Gaborone United katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

Aziz Ki Aweka Wazi Lengo la Yanga Dhidi ya Gaborone United: “Tunataka Kumaliza Kazi Ugenini” Kombe La Dunia U-20 Wanawake 2026: Uchambuzi wa Kundi A