Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika
Simba SC

Sababu Za Simba SC Kukiacha Kikosi Dar Kuelekea Malawi | Ligi ya Mabingwa

Vardo September 4, 2026 5:33 pm

Mabingwa wa soka nchini, Simba SC, wameweka wazi sababu za baadhi ya wachezaji wao nyota kutojumuishwa kwenye kikosi kilichosafiri nchini Malawi kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers.

Kikosi hicho chenye wachezaji 22 kiliondoka Dar es Salaam Alhamisi, Septemba 4, majira ya saa 1:00 asubuhi na kuwasili salama jijini Lilongwe majira ya saa 3:00 asubuhi chini ya Kocha Mkuu Steve Barker.

Wachezaji Walioachwa Kwa Majeraha Kocha na uongozi wamethibitisha kuwa kundi la kwanza la wachezaji limebaki Tanzania kuendelea na matibabu na kuuguza majeraha:

  • Shomari Kapombe (Nahodha)

  • Nickson Kibabage

  • Abdulrazak Hamza

  • Wilson Nangofi (Anaendelea na programu ya kurejea uwanjani)

  • Ya’kub Ali Sulaiman

Wachezaji Walioachwa Kwa Sababu Za Kiufundi Mbali na majeraha, wachezaji wengine watatu wameachwa Dar es Salaam kutokana na maamuzi ya mwalimu:

  • Kelvin Nashon

  • Daudi Semfuko

  • Ibrahim Nindi

Maandalizi ya Mchezo Nchini Malawi Baada ya kuwasili Lilongwe, wachezaji 22 waliosafiri wamepata muda wa kupumzika kabla ya kuanza mazoezi ya jioni kujiandaa na pambano hilo. Simba SC itashuka uwanjani Jumapili, Septemba 6, kupambana na Mighty Wanderers ikilenga kupata matokeo mazuri ugenini ili kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano na kufuzu hatua inayofuata.

Bahari Ya Burudani Yachafuliwa Na Wild White Whale Aziz Ki Aweka Wazi Lengo la Yanga Dhidi ya Gaborone United: “Tunataka Kumaliza Kazi Ugenini”