Home Uncategorized UONGOZI WA SIMBA WATAJA KILICHOWAKWAMISHA JAMHURI,MOROGORO

UONGOZI WA SIMBA WATAJA KILICHOWAKWAMISHA JAMHURI,MOROGORO

 


JANA mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba walibanwa mbavu kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Uongozi wa Simba umesema kuwa matokeo hayo yanaweza kuonekana sio mazuri kwa kuwa ni sare ila kutokana na mazingira ya miundombinu hamna namna ya kufanya.


Simba ilianza kufunga bao jana, Septemba 12 kupitia kwa kiungo mzawa, Mzamiru Yassin dakika ya 44 na liliwekwa sawa na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar dakika ya 46 Boban Ziringatus .

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:”Yaweza kuonekana matokeo sio mazuri kwa kuwa tumepata  sare. Kupata pointi nne away(ugenini) katika viwanja kama vile ni kitu cha kushukuru pia.”


Mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 2-1 mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine na mchezo wa pili imekwama kusepa na pointi tatu kama ilivyotokea kwa wapinzani wao Mtibwa Sugar kukwama, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

SOMA NA HII  HAJI MANARA: ZITAPIGWA GONGAGONGA NYINGI SANA LEO DHIDI YA NDANDA