Uncategorized

NYOTA ALIYEKUWA AKIWINDWA NA MANCHESTER UNITED AJIFUNGA MIAKA MITANO VILLA

admin September 16, 2020 9:47 pm


 KIUNGO fundi wa Aston Villa ambaye ni nahodha wa Mtanzania, Mbwana Samatta, Jack Grealish amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

 

Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka nane pekee amesaini mkataba huo ambao utamfanya aendele kusalia Villa kwa miaka mitano zaidi.

 

Na hivyo utamfanya kulipwa mshahara wa paundi 140,000 kwa wiki kutoka paundi 70,000 alizokuwa akizipata hapo awali.


Nyota huyo amesema “Ni klabu yangu, hapa ni nyumbani na najisikia furaha hapa,nina amini nitaendelea kushirikiana na wenzagu kwa ajili ya kufikia malengo ya timu kwa kushirikiana na wenzagu.”

 

Grealish alikuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktoba 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.

UCHEBE AMPOTEZA JUMLAJUMLA SVEN NDANI YA SIMBA YANGA YAJA NA MIFUMO MITATU YA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply