BAADA ya pazia la Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2020-21 (VPL), Ligi kuu ya Uingereza (EPL) pamoja na ile ya Italia maarufu kama Seria A kufunguliwa siku za hivi karibuni, Klabu ya Mbeya City, Juventus pamoja na Leicester City zaingia kwenye udhamini mpya na wa kipekee na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Parimatch inayoendesha shughuli zake nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana na kusema kwamba wamejipanga vilivyo katika kukuza na kuleta changamoto mpya kwenye soka la Tanzania kwa kuangalia katika kushirikisha vilabu vya ndani na nje ya nchi.
“Tunafuraha kubwa kutangaza kuwa washirika na Leicester City pamoja na Juventus, uhusiano huu utakuwa muhimu kwa pande zote kwa namna moja ama nyingine. Kiukweli hii ili kuwa ni ndoto yetu ya kipindi kirefu kuingia katika udhamini na klabu kubwa za kimataifa na sasa hilo tumelifanikisha na tumekuwa wa kwanza kuweka historia kwa Tanzania kufanya hivyo.
“Mbali na hayo, ni dhahiri tunaenda kuiona Mbeya City katika ‘level’ zingine ndani ya msimu huu licha ya kwamba, imeonekana kuanza kwa kususua katika mechi zake mbili za ufunguzi ilizocheza ugenini kati ya KMC na Yanga SC.
“Kila kitu ni muda na huenda mchezo unaofuata wa Septemba 20 dhidi ya Waoka mikate wa Vingunguti ‘Azam FC’ akavunja historia yake ya kufungwa na matajiri hao na kuanza kasi ya kutafuta ubingwa wa msimu huu, hakuna kinachoshindikana katika soka kila kitu ni jitihada na mbinu kali za kupambana na mpinzani,” amesema.
MBEYA CITY YAINGIA LEVEL ZA JUVENTUS NA LEICESTER CITY
Leo Mbeya City inakibarua cha kumenyana na Azam FC kwenye mchezo wa ligi utakapigwa majira ya saa 8:00 Uwanja wa Sokoine.