Uncategorized

DAVID MOYES, MENEJA WA WEST HAM UNITED AKUTWA NA CORONA

admin September 23, 2020 5:47 am


KOCHA Mkuu wa West Ham, David Moyes amekutwa na Virusi vya Corona pamoja na wachezaji wake wawili ambao ni Issa Diop na Josh Cullen.

West Ham ilipokea majibu hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa raundi ya tatu ya mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya Hull uliochezwa Jana, Septemba 22 Uwanja wa London.

Mchezo huo West Ham ilishinda kwa mabao 5-1 ambapo watupiaji walikuwa ni  Robert Snodgrass dk 18, Sebastian Haller 45,90+1 na Andry Yarmolenko 56,(p) na 90 lile la Hull City lilipachikwa na Mallik Wilks dk 70.

Taarifa kamili iliyotolewa na uongozi wa West Ham umethibitisha kwa kusema kuwa wachezaji hao pamoja na meneja wa timu hiyo wamekutwa na Virusi vya Corona kwa sasa wapo kwenye uangalizi.

 “West Ham United inathibitisha kwamba David Moyes, Issa Diop na Josh Cullen wamekutwa na Covid -19. Tunawawaombea warejee kwenye ubora wao na tutafuata taratibu zilizowekwa na Ligi Kuu England kwa ajili ya kujali afya zao na zetu pia.”

Kwenye mechi hiyo kocha msaidizi Alan Irvine alichukua majukumu ya kukiongoza kikosi hicho.

SIMBA YAPIGA HESABU ZA KUSHINDA MECHI ZOTE DAR ISHU YA NIDHAMU YA MORRISON NDANI YA SIMBA IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply