Home Uncategorized KISINDA:TUNA JUKUMU KUBWA KUTATIMIZA MALENGO

KISINDA:TUNA JUKUMU KUBWA KUTATIMIZA MALENGO

 


TUISILA Kisinda winga mpya ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wanajukumu kubwa la kupambana kwa ajili ya timu hiyo ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Kisinda ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo aliibukia kikosini akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo pamoja na nyota mwenzake Tonombe Mukoko. 


Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa raundi ya nne dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 27,Uwanja wa Jamhuri Morogoro. 


Kisinda amesema:”Wachezaji tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kutimiza majukumu yetu ndani ya Yanga pamoja na kuwapa furaha mashabiki.”

SOMA NA HII  BEKI MKENYA AJIPELEKA MWENYEWE SIMBA ASAINI