Home Uncategorized VITA YA KIATU CHA UFUNGAJI BORA NI MOTO NDANI YA LIGI KUU...

VITA YA KIATU CHA UFUNGAJI BORA NI MOTO NDANI YA LIGI KUU BARA

 


IKIWA kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara ni mzunguko wa nne umekamilika huku zikichezwa jumla ya mechi nne ile vita ya kuwania kiatu bora kwa upande wa ufungaji bora inazidi kupamba moto.


Kwa sasa tuzo hiyo ipo mikononi mwa Meddie Kagere ambaye msimu wa 2019/20 alitupia jumla ya mabao 22 na timu yake ya Simba ilitwaa ubingwa wa ligi.


Kazi imeanza msimu huu ambapo kwenye vita hiyo mambo yapo namna hii:-


Prince Dube wa Azam FC yeye ni namba moja akiwa ametupia mabao matatu, mabao mawili aliwatungua Coastal Union Uwanja wa Azam Complex na bao moja aliwatungua Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela.


Meddie Kagere wa Simba yeye ana mabao mawili aliwafunga Biashara United na Gwambina FC ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Clatous Chama wa Simba ana mabao mawili aliwafunga Biashara United Uwanja wa Mkapa.


Chris Mugalu  wa Simba yeye ana mabao mawili aliwafunga Biashara United na Gwambina FC ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Mzamiru Yassin wa Simba ana mabao mawili aliwafunga Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri na Ihefu FC Uwanja wa Sokoine.


Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania aliwatungua mabao mawili Dodoma Jiji. 


Reliats Lusajo wa KMC aliwatungua mabao mawili Mwadui FC, Uwanja wa Mwadui Complex.


Bigirimana Blaise, aliwatungua bao moja Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani na Mbeya City Uwanja wa Sokoine.


Lamine Moro wa Yanga aliwatungua bao moja Mbeya City na bao moja Mtibwa Sugar.


Hassan Kabunda wa KMC ana mabao mawili aliwatungua Mbeya City na Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA MAANGAMIZI CHA NDANDA FC MSIMU WA 2019/20