Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA BIASHARA UNITED

RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA BIASHARA UNITED

[the_ad id="25893"]

 


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara msimu mpya wa 2020/21 kwa timu zote ambazo watakutana nazo ndani ya uwanja.


Ruvu ilifungua pazia lake kwa kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Mtibwa Sugar kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ihefu na kuibukia Mabatini kwa kushinda bao 1-0 mbele ya Gwambina FC.

Bao hilo la ushindi la kwanza kwa Ruvu Shooting msimu wa 2020/21 lilipachikwa na nahodha Fully Zully Maganga baada ya kuyeyusha dakika 220 bila kuambulia bao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa hawana mashaka na maandalizi ya kikosi chao kwa kuwa inajulikana ni Barcelona ya Bongo.

“Ipo wazi sisi ni Barcelona ya Bongo hasa kwenye soka tunapiga pasi nyingi balaa hasa ukitukuta tupo pale Mabatini hata tukiwa nje tunapiga mpira mwingi.

“Mfano mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar pale Morogoro wakati tunalazimisha sare sisi tulimiliki mpira kwa asilimia kubwa hivyo tunajiamini, mchezo wetu unaofuata tunahitaji ushindi kwenye mechi zetu zote,” amesema.

Ruvu itamenyana na Biashara United Septemba 27 Uwanja wa Mabatini majira ya saa 8:00 mchana.
SOMA NA HII  VODACOM WAREJEA LIGI KUU BARA KWA MASHARTI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here