YUSUPH Mhilu mtupiaji namba moja ndani ya Kagera Sugar ana kibarua kizito cha kuongoza kikosi chake kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Oktoba 4, majira ya saa 1:00 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa inakutana na timu ambayo haijapoteza mchezo kwenye mechi nne za msimu huu.
Bao lake la kwanza aliwatungua KMC Septemba 25 Uwanja wa Kaitaba na kuwafanya wapoteze mchezo wa kwanza Kaitaba kwa kuwa ilikuwa imecheza mechi tatu bila kupoteza.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya mbele ya Azam FC hivyo watapambana kusaka pointi tatu muhimu.
“Utakuwa mchezo mgumu kwetu na wapinzani wetu ni timu nzuri tutapambana kupata matokeo mashabiki watupe sapoti,” amesema.
Mhilu msimu wa 2019/20 alitupia jumla ya mabao 13 kwa sasa akaunti yake ina bao moja kibindoni.