Uncategorized

AZAM FC WAFAFANUA SABABU YA CHIRWA KUACHWA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA

admin October 9, 2020 8:47 am

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa suala la nyota wao Obrey Chirwa kuachwa na timu ya Taifa ya Zambia, amesababisha yeye mwenyewe.


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia, Milutin Sredojevic, ‘Micho’ aliwaacha nyota wawili ambao wanacheza ndani ya Ligi Kuu Bara.


Nyota mwingine ni Clatous Chama wa Simba ambaye naye ni miongoni mwa walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia.


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema:” Suala la Chirwa uraratibu wote wa safari ulikuwa sahihi na baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Oktoba 4, Chirwa alipaswa kusafiri Oktoba 5 lakini alichelewa ndege licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa kuwahi.”


Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Chirwa kuitwa timu ya Taifa ya Zambia kwa kuwa alikuwa hajawahi kuitwa kuitumikia timu hiyo zaidi ya kuishia kwenye timu za chini ya miaka 20.


Ndani ya Ligi Kuu Bara, Chirwa ametupia jumla ya mabao mawili na ana pasi moja ya bao.

YANGA KIGELEGELE AWAOMBA MASHABIKI KUACHA MIHEMUKO MRITHI WA MIKOBA YA ZLATKO APEWA MAJUKUMU MAWILI NDANI YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply