KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi leo Oktoba 23 kimewasili salama Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 25 Uwanja wa CCM Kirumba saa 10:00 jioni.
Tayari wenyeji wa mchezo huo ambao ni KMC walishatia timu Mwanza wakitokea Dar, Oktoba 22.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wachezaji wote wapo salama na ni mchezaji mmoja ambaye amebaki Bongo ambaye ni Mapinduzi Balama kwa kuwa bado afya yake haijatengamaa.
“Kikosi kipo salama na wachezaji wote wapo vizuri, ni mchezaji mmoja ambaye hayupo kwenye orodha kwa kuwa bado afya yake haijatengamaa na mwalimu ameshauri abaki kwa kuwa hataweza kumtumia ni Mapinduzi Balama.
“Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.
KMC inashuka uwanjani ikiwa inakumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru inakutana na Yanga iliyotoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru.