Home Uncategorized RUVU SHOOTING: UWEZO WA SIMBA NI MDOGO,PIRA BIRIANI SASA LITAKUWA KACHORI

RUVU SHOOTING: UWEZO WA SIMBA NI MDOGO,PIRA BIRIANI SASA LITAKUWA KACHORI

 


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa uwezo wa timu ya Simba inayojiita ina kikosi kipana ndani ya uwanja ni mdogo jambo ambalo liliwafanya wawafunge bao 1-0 Uwanja wa Uhuru, Oktoba 26.


Ruvu Shooting iliendelea kupiga pale ambapo Simba iliumia baada ya kutoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulichezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela.


Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa walijipanga kwa muda mrefu kwa kuwa timu imekuwa na maandalizi mazuri jambo ambalo walitarajia ilikuwa ni kupata pointi tatu.


“Nadhani Watanzania wameshuhudia namna ambavyo tulicheza mpira mkubwa na mwingi ndani ya uwanja bila kuwaudhi wale ambao walilipa kiingilio.


“Sasa hapo unaona wazi kwamba mpira wa Simba ni mdogo hawana uwezo mkubwa katika kucheza kwa wachezaji wao. Wanatamba wana kikosi kipana wanacheza pira biriani ninaamini limegeuka kuwa pira kachori.


“Sera yetu ni ileile ya kupapasa na kukung’uta ili kupata pointi tatu, tupo vizuri vijana wanalipwa kwa wakati, msosi kabisa wanakula vizuri na wanapikiwa na wapishi maalumu unadhani nini kitatokea ndani ya uwanja?


Ruvu Shooting ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi nane huku Simba ikiwa nafasi ya nne na pointi zake ni 13 baada ya kucheza mechi saba.


Baada ya Ruvu Shooting kuitungua Simba na kufanya ipoteze mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180, nahodha wa Simba John Bocco aliomba msamaha kwa mashabiki wa Simba.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAIPIGA MKWARA MZITO ALAHLY