Uncategorized

LIVERPOOL YABAMIZA MTU MKONO

admin November 4, 2020 7:47 am


 MECHI za hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu 2020/21 zimeendelea kuchezwa kwenye viwanja mbalimbali.

Usiku wa jana Novemba 3 2020, zilichezwa jumla ya mechi nane na kushuhudia vipigo vizito.


  Ni mechi  tatu pekee ndizo zimemalizika kwa ushindi wa magoli mengi ambapo ni mechi ya Shakhtar wakiwa nyumbani wamefungwa 0-6 na Mönchengladbach, RB Salzburg wakiwa nyumbani kwao wamefungwa 2-6 na Bayern Munich huku Liverpool nao wakiwa ugenini wameichapa Atalanta 5-0.


Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa anaona vijana wake wanafanya yale ambayo mashabiki wanahitaji pamoja na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.


“Ninaona vijana wangu wanafanya kile ambacho tunahitaji kupata ndani ya uwanja ambacho ni ushindi, hata mashabiki pia wanahitaji kuona timu inashinda.


“Bado kazi ipo na tuna jukumu la kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo, uwezo upo na sapoti ni kubwa,” amesema.

KOCHA YANGA ATOA TAMKO KUHUSU POINTI MOJA JINA LA DULLA MBABE LAONDOLEWA LKWENYE PAMBANO, SABABU ZATAJWA, ITABA NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply