Uncategorized

CLATOUS CHAMA AITWA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA

admin November 10, 2020 9:47 am

 


NYOTA wa Klabu ya Simba, Clatous Chama ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Zambia ili akaitumike timu yake hiyo maarufu kama Chipolopolo.


Kwa sasa timu ya Zambia ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu Afcon ambapo itamenyana na Botswana, Novemba 12 nchini Zambia.


Kiungo huyo ambaye amekuwa kwenye ubora ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21 akiwa na pasi tano za mabao pamoja na kufunga mabao mawili ameitwa baada ya Enock Mwepu kuwa ‘locdown’.


Kiungo huyo anatumika ndani ya Klabu ya Red Bull Salzburg kutokana na wachezaji wa timu hiyo sita kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

SAMATTA KUIKOSA TUNISIA NOVEMBA 13 MWALIMU KASHASHA AIPA PONGEZI GLOBAL GROUP, AWATAJA WATATU WACHAPAKAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply