Uncategorized

MO DEWJI AWATULIZA SIMBA, AWAAMBIA CHAMA ANA MKATABA MREFU SIMBA

admin November 15, 2020 11:47 am




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema klabu hiyo ilishaingia mkataba mpya na kiungo Cleotus Chama.


Mo Dewji amesema mkataba wao na Chama unaisha mwaka 2022, hivyo taarifa za kuwa anakwenda Yanga zimekuwa zikiwashangaza.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema mchezaji huyo ni mali ya Simba na hakuna sababu ya kuwa na hofu.


“Taarifa sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana.


“Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni mchezaji wa Simba.


“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka wapi lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,” alisema Mo Dewji.


MO DEWJI AFUNGUKA KUHUSU MUKOKO TONOMBE, ASEMA MWALIMU KAPELEKA MAPENDEKEZO YA KIUNGO MKABAJI YANGA YAJIPIGIA AFRICAN LYON MABAO 3-1

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply