Uncategorized

POGBA AKIRI KUPITIA MAISHA MAGUMU NDANI YA MANCHESTER UNITED

admin November 17, 2020 7:47 am


 KIUNGO wa kati wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba, anasema kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana cha kazi yake ya soka kutokana na muda wake wa mchezo katika Old Trafford.


Nyota huyo kwa sasa hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer jambo linalomfanya afikirie kusepa ndani ya kikosi hicho.


Habari zinaeleza kuwa mabosi wa United kwa sasa wapo tayari kumuuza nyota huyo anayecheza timu ya Taifa ya Ufaransa.

Akifanyiwa mahojiano na kituo cha RTL Pogba  amesema kuwa; “Napitia kwenye wakati mgumu sana kuliko wakati wowote ule katika maisha yangu ya soka.  Timu ya taifa ndiyo imekuwa kama pumzi ya mimi kuja kupumulia huku, ni mahali safi, nafurahia zaidi,”.

KOCHA SIMBA APIGWA CHINI JUMLAJUMLA MO AJA NA MKAKATI KWA AJILI YA SIMBA QUEENS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply