Uncategorized

SAKATA LA BERNARD MORRISON NA YANGA LAIBULIWA UPYA KABISA

admin November 20, 2020 9:47 am

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa una wasiwasi kuhusu kesi ya mchezaji wao Bernard Morrison huenda ikabadilishwa kwa kuwa dirisha dogo la usajili linakuja na hakuna walichopokea kuhusu malalamiko yao.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba Yanga waliripoti kwamba Morrison mkataba wake haujakamilika kwa kuwa kuna sehemu hazijajazwa na wahusika jambo linalomaanisha kwamba mkataba wake ni feki.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanamashaka na kesi yao hiyo ambayo haijaskilizwa huenda mabadiliko yakafanyika kwenye mkataba dirisha dogo la usajili likifika.


“Kesi yetu kuhusu Morrison tulipeleka malalamiko kwa wahusika na mpaka sasa hakuna tulichokipata, wasiwasi wetu ni kwamba ikifika Desemba 15 dirisha dogo la usajili likifunguliwa huenda wakafanya mabadiliko.


“Kwenye mkataba wa mchezaji Morrison sisi tuliweka wazi kwamba kuna sehemu hazijazijajazwa hivyo huenda wakatumia mwanya huo kwenye dirisha dogo kuziba mapengo, maombi yetu ni kwamba shauri let lisikilizwe na lifanyiwe kazi,” amesema Mwakalebela wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda huu makao makuu ya Yanga.

HARUNA NIYONZIMA WA YANGA APATA AJALI VITA YA COASTAL UNION V SIMBA BALAA TUPU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply